Kinyozi mmoja nchini Kenya anaefahamika kwenye mitandao kama Chief Safro, ameendelea kujizolea umaarufu ndani na nje kwa kutumia zana za jadi kama beleshi na tindo kunyoa nywele, mtindo ambao umemsaidia kujipatia wafuasi lukuki kwenye mitandao yake ya kijamii kama Instagram na TikTok ambapo wanafika zaidi ya milioni moja.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Safari Martins, mzaliwa wa Rwanda anayefanya kazi zake jijini Nairobi, amekuwa maarufu na kuwa na ushawishi mkubwa kwenye sekta ya uonyoaji nywele, akitumia vifaa ambavyo kawaida ungeweza kuviona vikitumika kwenye kilimo na useremala.

Duka lake la kinyozi liko kando na barabara katika kaunti ya Kiambu nje kidogo ya jiji la Nairobi, ambapo Martins anachanganya ujuzi, fasihi za kitamaduni na mitindo ya nywele ili kuvutia wateja na watazamaji mtandaoni.

Mbinu za Martins za kunyoa nywele, kama vile beleshi, tundo na vifaa vingine vilivyochongoka, ni sehemu muhimu ya mvuto wake mtandaoni, video za namna akinyoa nywele hurekodiwa na msaidizi wake na hushirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mara nyingi huvutia mamia ya maelfu ya watu.

Safari anasema “Ninavutiwa na na utamaduni wa kiafrika na hadhiri za Afrika”, akisema baadhi ya vifaa anavyovitumia ni vya kipekee na vimetokana na tamaduni mbalimbali, akisisitiza kuwa moja ya kifaa anachotumia kunyolea kilipewa baraka na wazee wa Kijiji.

Safari Martins anatumia mbinu za jadi kunyoa nywele
Safari Martins anatumia mbinu za jadi kunyoa nywele AP – Andrew Kasuku

Mmoja ya wateja wake ni Ian Njenga, ambaye anasema ufundi wa Martin ndio unaomtofautisha na vinyozi wengine na kwamba uamuzi wa Kwenda kwenye saluni yake ulitokana na ushawishi alionao kwenye mitandao ya kijamii.

Martin anatoza shilingi za kenya 1500 ambayo ni sawa na dola 12 kila anapomnyoa mtu, kiwango hiki kikiwa ni chajuu ukilinganisha na bei za saluni nyingine za kunyoa za wanaume, ambapo bei ya chini kabisa inaazia shilingi ya 150.

Wateja wake wengi wanasema hadhi yake na namna anavyonyoa ndiko kunamfanya Martin awe wa tofauti lakini pia kuhusishwa kwenye mitandao yake ya kijamii.

Vinyozi wenye ushawishi wamekuwa wakiongezeka nchini Kenya, ambapo matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kulingana na kampuni ya utafiti wa masoko DataReportal, Kenya ilikuwa na watumiaji milioni 10.6 wa mitandao ya kijamii mwezi Januari 2023, na kufikia Januari 2025, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi milioni 15.1, ongezeko la karibu asilimia 50.

Safari Martins akiwa na mteja wake kwenye sehemu yake ya kazi.
Safari Martins akiwa na mteja wake kwenye sehemu yake ya kazi. AP – Andrew Kasuku

Ukuaji huu umetengeneza fursa mpya za mapato, hasa kwa watengenezaji wa maudhui ya mtandaoni.

Mfano mzuri ni muhtasari uliochapishwa mwezi Juni mwaka uliopita uliofanywa na Taasisi ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera za Umma nchini Kenya, ambapo uliripoti kwamba takriban asilimia 15 ya Wakenya wanaohusika katika utengenezaji wa maudhui mtandaoni wanategemea sekta hiyo kama chanzo chao kikuu cha mapato, hata hivyo Martin anasema kiuhalisia vinyozi wabunifu mtandaoni wanapata fedha pungufu na watengenezaji wa maudhui kidijitali.

Hata hivyo pamoja na changamoto anazopitia, Martins anaendelea kukuza chapa yake kwa kuchanganya fani ya unyoaji nyweli na simulizi za hadithi za kidijitali, akionyesha jinsi uchumi bunifu wa Kenya unavyobadilika pamoja na kupanuka kwa wigo wa majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *