Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba, Jamary Abdul amewataka vijana kote nchini kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi.

Jamary amesema hayo huo leo Januari 2, 2026 alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya Kimtaifa ya Biashara Zanzibar yanayoendelea katika viawanja vya Dimani mjini Magharibi Zanzibar.

Jomary ameipongeza VETA kwa kuendelea na jitihada za kupanua mafunzo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani vijana sambamba na hilo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika mafunzo ya ufundi stadi .

“Baada ya kutembelea banda la VETA hapa kwa kweli nimeona kuna fursa nzuri lakini pia kazi za mikono, nahii inaonesha tija kwamba vijana wanaohitimu elimu ya sekondari hata wakishindwa Kwenda vyuo vya kati na vikuu wanayonafasi ya kujiunga na vyuo vya VETA na hatimae kupata ujuzi na kuweza kujiajiri”.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi inashiriki katika maonesho ya kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) yaliyoanza tarehe 29 Desemba na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 16 Januari, 2026.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *