Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, amesema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya wanafunzi wa elimu ya awali, msingi na sekondari kushindwa kukamilisha masomo yao, hali inayodhoofisha maendeleo ya sekta ya elimu.

Akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufunuo wilayani Kahama, Nkinda amesema changamoto hiyo inachangiwa na sababu mbalimbali, zikiwemo malezi duni kutoka kwa wazazi na ukosefu wa ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya watoto kielimu.

Ameeleza kuwa watoto wengi huanza masomo wakiwa na ari kubwa, lakini wanapofikia darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne, idadi kubwa huacha shule au kupotea kabisa katika mwelekeo wa kielimu.

✍Kasisi Kosta
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Kasisi Kosta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *