Jamii ya Kiislamu Afrika Mashariki na hasa nchini Tanzania imekumbwa msiba mkubwa kufuatia kufariki dunia kwa mwanazuoni mashuhuri, na mfasiri wa Qur’ani Tukufu, Sheikh Ali Jumaa Mayunga, aliyefariki dunia leo tarehe 1 Januari 2026, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Marehemu Sheikh Ali Jumaa Mayunga alikuwa miongoni mwa wanazuoni waliotumia maisha yao yote katika kuhudumia dini ya Kiislamu, kuutetea ukweli wa Ahlulbayt (AS), pamoja na kuwaelimisha Waislamu kupitia mihadhara, maandiko na tafiti za kina za kielimu.

Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania TIC Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge ameongoza Swala na Majlis ya Al-Marhum Sheikh Ali Juma Mayunga ambaye pia alikuwa mwandishi wa vitabu kadhaa

Sheikh Ali Manyunga atakumbukwa na mengi hasa Umahiri wake na weledi wa kutafsri Qur’an Tukufu ambayo imewaongoza watu wengi.

Sheikh Ali Mayunga amezikwa leo katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, Dar es Salaam.

Sheikh Mayunga alizaliwa Mwaka 1947 Mkoa wa Tabora katika Wilaya ya Igunga Tarafa ya Simbo na ni miongoni mwa wanafunzi wa Marhum Sheikh Mzee Fereji Farahani wa mkoa wa Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *