Gazeti moja la nchini Uingereza limeufungua mwaka mpya wa 2026 kwa ripoti kuhusu wasiwasi juu ya hali ya mashindano ya Kombe la Dunia ya mpira wa miguu mwaka huu 2026 na kusema kuwa rais wa Marekani Donald Trump ni tatizo kubwa kwa mashindano hayo.

Shirika la habari la FARS limeripoti habari hiyo na kulinukuu gazeti la Athletic na kuandika kwamba, moja ya wasiwasi mkubwa wa ripoti ya jana Alkhamisi ya gazeti la Athletic katika mwaka mpya wa 2026 ilikuwa vipi Trump atatekeleza ahadi zake kuhusu michuano ya Kombe la Dunia la mpira wa miguu mwaka huu wa 2026.

Kwa mujibu wa gazeti la Politico, Trump ametoa ahadi zaidi ya 200 katika vipindi vyake viwili vya urais, lakini nusu ya ahadi zake hajazitimiza.

Katika muhula wake wa kwanza, Trump aliposhinda kuandaa Kombe la Dunia, alijigamba kuwa ataandaa Kombe la Dunia ambalo watu wote wangelihudhuria, lakini ahadi hiyo hakuitimiza.

The Athletic limeandika pia kwamba, uhusiano wa karibu wa Infantino na Trump umefanya Trump apate kisingizio rahisi cha kuvunja ahadi zake.

Kwa mujibu wa New York Times, uasi wa kwanza wa Trump kwenye Kombe la Dunia ulikuwa wa kuwapiga marufuku watazamaji kutoka Iran, Senegal, Haiti na Ivory Coast wasiende kwenye michuano ya nchini Marekani.

Mpaka muda huu Trump hajatekeleza ahadi zake nne kuu: ambazo ni kupunguza bei za chakula na gharama za maisha huko Marekani, kukomesha vita nchini Ukraine ndani ya saa 24, kupunguza bei ya petroli hadi chini ya dola 2, na kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico kama alivyoahidi kwenye muhula wake wa kwanza wa urais.

Montagliani, rais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini, anasema kwamba siasa kali za Trump ndiyo sababu ya kuvuruga upatikanaji wa visa na usalama wa wageni, jambo ambalo linapingana na ahadi ya Trump ya kutofanya ubaguzi kwa wanamichezo na mashabiki na jambo hilo linaweza kuharibu umaarufu na imani ya walimwengu kwa mashindano hayo.

Kwa upande wake gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika kwamba katika tukio la matumizi ya lugha mbaya ya mwenyeji wa Kombe la Dunia, mashirika ya kimataifa ya haki za watazamaji yanapaswa kuhakikisha lugha hizo mbaya zinapungua sana kupitia kuanzisha kampeni kubwa ya kukabiliana nazo, kuwasilisha malalamiko kwa FIFA, na kutumia vizuri nguvu za vyombo vya habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *