Wakazi wa mkoa wa njombe wamesherekea mwaka mpya na siku ya vikasha kwa kupanda miti katika kijiji cha Lusitu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Zoezi hilo linalenga pia kuimarisha vyanzo vya Maji ili kupata Maji ya Uhakika kwa Wananchi wa Jimbo la Njombe Mjini

Licha ya Mkoa wa Njombe Kupata Miradi ya Maji yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 60 lakini tahadhari imetolewa kwa wananchi kuendelea kulinda vyanzo vya maji kwa kutokata miti ovyo na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

Marry Ulasa Kutoka Ofisi ya Mazingira halmashauri ya mji njombe amesema wanaendelea kushirikiana na ofisi za vijiji katika kuhimiza upandaji miti na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Wananchi wa Kijiji cha Lusitu Wamesema Moja chanzo cha vyanzo vya Maji Kuharibika ni uwepo wa miti isiyo rafiki katika Vyanzo vya Maji, huku wakipongeza hatua na mbunge wa njombe mjini Deo Mwanyika kwa kwa kushiriki na wakazi wa kijiji hicho kusherehekea sikukuu za mwaka mpya na siku ya vikasha, kupanda miti katika vyanzo vya maji.

Zaidi ya miti elfu tatu (3,000) imepandwa na bado zoezi hilo ni endelevu.

Zoezi la Kutunza vyanzo vya Maji Kwa Jimbo la Njombe Mjini na Mkoa wa Njombe linasimamiwa na Viongozi wa serikali kwa Kushirikiana na Wananchi Ili Kuhakikisha Miti Inayo Pandwa Inalindwa na Kutunzwa.

Mwandishi @dkhan1410
#RFAOnline
@HabariStartv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *