Zohran Mamdani ametangazwa kuwa meya mpya wa Jiji la New York City, nchini Marekani na hivyo kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi kuliongoza jiji hilo tangu mwaka 1992. Aidha, anakuwa meya wa kwanza Muislamu, aliyezaliwa barani Afrika, kushika nafasi hiyo ya uongozi.

Akizungumza kwenye Morning Trumpet leo, mchambuzi wa masuala ya siasa, Ibrahim Rahbi mesema ujio wa Mamdani unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika siasa za jiji hilo.

Ameeleza kuwa tofauti na viongozi waliopita, Mamdani alichangiwa na wananchi wa kawaida, na si matajiri au watu wenye ushawishi mkubwa wa kifedha.

✍ Ibrahim kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *