Umoja wa Ulaya unasimama na raia wa Venezuela na unaunga mkono mpito wa amani na kidemokrasia nchini, amesema Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen siku ya Jumamosi, kufuatia kukamatwa kwa rais wa Venezuela na Marekani. “Tunafuatilia hali ilivyo nchini Venezuela kwa karibu sana.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tunasimama kwa mshikamano na raia wa Venezuela na tunaunga mkono mpito wa amani na kidemokrasia.” “Suluhisho lolote lazima liheshimu sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa,” umesema ujumbe kutoka kwa Ursula von der Leyen uliorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Lula analaani “shambulio kubwa dhidi ya uhuru wa Venezuela”

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amelaani siku ya Jumamosi “shambulio kubwa dhidi ya uhuru wa Venezuela” kufuatia shambulio la mabomu la Marekani huko Caracas mapema asubuhi na kukamatwa kwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, tangazo lililotolewa na Donald Trump. “Mashambuli na milipuko kwa eneo la Venezuela na kukamatwa kwa rais wake kunazidi mipaka ya kile kinachokubalika” na kutishia “kuhifadhiwa kwa eneo hilo kama eneo la amani,” Lula amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X. Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, kupitia Umoja wa Mataifa, “kujibu kwa nguvu” mashambulizi haya.

Mexico inalaani shambulio la kijeshi dhidi ya Venezuela

Mexico imelaani shambulio la Marekani dhidi ya Venezuela siku ya Jumamosi, ikionya kwamba “hatua yoyote ya kijeshi inahatarisha sana utulivu wa kikanda.” “Serikali ya Mexico inalaani na kukataa kwa nguvu zote vitendo vya kijeshi vilivyofanywa kwa upande mmoja katika saa za hivi karibuni na vikosi vya Marekani dhidi ya malengo yaliyo ndani ya eneo la Jamhuri ya Venezuela,” Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa.

Moscow yadai ufafanuzi “mara moja” kuhusu Hali ya Maduro

“Tumeshtushwa sana na ripoti kwamba Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe waliondolewa kwa nguvu kutoka nchini humo kufuatia uchokozi wa Marekani leo,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika taarifa, ikitaka “ufafanuzi wa haraka kuhusu hali hii.”

“Lazima sote tuheshimu sheria za kimataifa,” Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema

“Ningependa kuzungumza na Rais (Trump)… lakini kwa sasa, nadhani tunahitaji kuthibitisha ukweli,” Waziri Mkuu amesema katika taarifa fupi iliyorushwa kwenye televisheni ya Uingereza. Uingereza “haikushiriki katika operesheni hii… na ninaamini kabisa kwamba sote tunapaswa kuheshimu sheria za kimataifa,” ameongeza.

Maduro atakabiliwa na mashtaka ya dawa za kulevya na ugaidi, kulingana na Wizara ya Sheria ya Marekani

Utawala wa Trump umeangaza leo Jumamosi kwamba kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro, na mkewe watakabiliwa na “nguvu kamili ya mfumo wa haki wa Marekani” kuhusiana na mashtaka ya biashara haramu ya dawa za kulevya na ugaidi.

Waziri wa Sheria Pamela Bondi ameelezea kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba Nicolas Maduro na mkewe, ambao hawajulikani walipo, “hivi karibuni watakabiliwa na nguvu kamili ya vyombo vya sheria vya Marekani, katika ardhi ya Marekani, mbele ya mahakama ya Marekani.” Bondi amebainisha kwamba Maduro walikuwa na mkewe wameshtakiwa katika mahakama ya shirikisho ya New York kwa mashtaka ya “ugaidi wa dawa za kulevya” na “njama ya kuingiza kokeni” nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *