Mapigano makali yamejiri leo Jumamosi kati ya waasi wa wenye silha wa kundi la M23 na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Kinshasa katika miji kadhaa karibu na mji wa Uvira, mashariki mwa DR Congo, vyanzo vya ndani vilisema.

Eneo lenye utajiri mkubwa wa maliasili la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo linapakana na Rwanda na Burundilimekumbwa na mchafuko yanayoendelea kwa miaka 30 sasa.

Hali ya eneo hilo imezidi kuwa mbaya tangu mwaka 2021 kufuatia hujuma za waasi wa M23. 

Baada ya kuteka miji miwili mikuu ya mashariki ya Goma na Bukavu mwishoni mwa mwaka jana, kundi hilo lilianzisha mashambulizi mapya mwezi wa Desemba mwaka jana katika jimbo la Kivu Kusini na kufanikiwa kudhibti mji wa Uvira tarehe 10 Desemba. Uvirani mji wa kistratejia wenye jamii ya watu wapato ladhaa kadhaa unaopakana na Burundi nchi muitifaki wa Kongo. 

Waasi wa M23 pia waliyadhibiti maeneo kadhaa ya mipakani wakati serikali ya Kongo na Rwanda zilizpokuwa zikisaini mkataba wa amani huko Washington. 

Kelvin Bwija Mratibu wa Jumuiya ya KIraia katika mji wa Uvira ameeleza kuwa tangu leo alfajiri kumeripotiwa mapigano makali kati ya kundila M23 na wanamgambo kwa jina la Wazalendo wanaoiunga mkono serikali ya Kinshasa na jeshi la Kongo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Uvira. 

Ameyataja maeneo yaliyokumbwa na mapigano huko Uvira kuwa ni Kashombe, Lubanda, Musingwe,, Katongo na Kigongo. 

Wakati huo huo Luteni Reagen Mbuyi Kaloni Msemaji wa kikanda wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amethibitisha kujiri mapiganokati ya pande mbili hizo huko Kigongo na Katongo hasa katika miinuko ya Kashombe na Lubanda katika mji wa Uvira. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *