MOROCCO; TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo Januari 4, 2026 itashuka Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat kuwavaa wenyeji Morocco hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) kweny.
Morocco walimaliza kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi saba, huku Taifa Stars wakiwa nafasi ya tatu katika Kundi C ikiwa na pointi mbili, wakiibuka kati ya timu zilizoshika nafasi za washindwa watatu bora.
Taifa Stars ilifungwa na Nigeria 2-1 katika mchezo wa kwanza, kabla ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda na Tunisia.
Morocco ‘Simba wa Atlas’ waliichapa Comoro mabao 2-0, sare ya 1-1 na Mali na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Zambia.
Jana Serikali ya Tanzania iliizawadia Taifa Stars kiasi cha Sh milioni 500, kufuatia kufuzu hatua ya 16 Bora katika michuano ya AF CON 2025.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Sh milioni 500 kwa timu kufuzu hatua hiyo, na ameahidi kutoa za wadi nono timu itakapoitoa Morocco na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
“Nianze kwa kuwaponge za kwa hatua mliyofanya, niwafikishie salamu za rais anawapongeza sana. Serikali inatambua masuala ambayo serikali inapaswa kukamili sha na mengine yashaanza kutelekezwa, amenituma niwafikishie salamu za pongezi, zimetangulizwa Shilingi milioni 500,” alisema Dk Mwigulu.
Dk Mwigulu alisema rais amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.
Aidha, Dk Mwigulu aliongeza kuwa, Rais Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali.
