
Mamlaka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zinadai kuwa na ushahidi mpya unaothibitisha uwepo wa jeshi la Rwanda mashariki mwa nchi, hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, wakisaidia waasi wa AFC/M23.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Siku ya Jumamosi hii, Januari 3, vikosi vya jeshi vya Kongo viliwaonyesha wanajeshi kumi na watano wa Rwanda waliohusishwa na uasi kwa vyombo vya habari, waliokamatwa katika vitani katika maeno mbalimbali. Kundi hilo pia linajumuisha raia wa kigeni. Taarifa hii inakuja wakati mapigano yakiendelea. Licha ya mipango ya kidiplomasia na kusainiwa kwa mikataba hivi karibuni iliyokusudiwa kusafisha njia ya kupunguza mzozo, mapigano yanaendelea karibu na mji wa kimkakati wa Uvira.
Wakiwa wamenyoa vichwa na wamevaa sare za gereza za njano na nyekundu, wafungwa hao walionyesha kwa vyombo vya habari. Luteni Kanali Mak Hazukay, naibu mkuu wa idara ya mawasiliano ya jeshi la Kongo, alikuwa na msimamo mkali: “Rwanda inaendelea kudumisha jeshi lake katika eneo la Kongo. Kuendelea kukaliwa kwa Uvira, iliyoko mbali na mipaka yake, kunathibitisha kwamba sababu iliyotolewa na Kigali kwa hatua za kujilinda ni uongo mtupu.”
Kundi la wanajeshi wa Rwanda walionyeshwa kwa vyombo vya habari lilikuwa linaongozwa na maafisa wawili wa vyeo vya meja na kepteni. Kulingana na Kinshasa, wote ni maafisa wa ujasusi. Maafisa hawa walikamatwa karibu na mji wa Goma, huku wanajeshi wengine wa ngazi ya chini wakikamatwa na jeshi la Kongo huko Kivu Kusini.
Raia pia walikamatwa
Raia mmoja wa Burundi huko Kinshasa, wengine watatu kutoka Burundi walikamatwa Uvira, Mganda mmoja huko Kivu Kaskazini, na Watanzania watatu. Wanashtakiwa kwa ugaidi, kutetea ugaidi, na ujasusi: “Imebainika kwamba kwa kutumia baadhi ya raia kutoka nchi za kanda hii na makundi yenye silaha kama Red-Tabara, Kigali inatafuta kuufanya mgogoro huu uwe wa kikanda,” chanzo cha kijeshi kimeongeza.
Hii si mara ya kwanza Kinshasa kuonyesha wanajeshi wa Rwanda waliokamatwa. Kila wakati, Kigali inakataa shutuma hizo. Mamlaka ya Rwanda inakubali tu kile wanachokiita “hatua za kujilinda” ili kujilinda dhidi ya waasi wa Kihutu wa FDLR na vikosi vingine hasimu.