Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, linasema vikosi vya usalama nchini Uganda vimetumia njia za mateso na ukamataji usio wa kisheria kuwatisha wapinzani kuelekea uchaguzi wa Januari 15.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu mamlaka zikikanusha madai ya kuwa na mpango wa kuzima hudma ya mtandao wakati wa uchaguzi.

Amnesty inasema imekusanya ushahidi unaoonesha maofisa usalama wakiwapiga na kutumia gesi za machozi dhidi ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani NUP kinachoongozwa na Robery Kyagulani maarufu kama Bob Wine.

Ripoti ya Amnesty imetolewa wakati huu mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda, Nyombi Thembo, akikanusha madai kuwa watazima mtandao siku ya uchaguzi.

Kauli yake imekuja huku wizara ya mawasiliano ikioya vyombo vya Habari vitakavyorusha maudhui ya vurugu kuelekea na siku ya uchaguzi.

Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81 hivi sasa ni miongoni mwa wagombea kwenye uchaguzi wa Januari 15 ambao anajaribu kuongeza utawala wake wa miaka 40, mpinzani wake mkuu akiwa ni Bob Wine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *