Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodríguez, ameomba uhusiano mzuri na wa heshima na Marekani siku ya Jumapili wakati wa mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri, akialika Washington “kufanya kazi pamoja katika ajenda ya ushirikiano.” Akiwa amezuiliwa katika gereza la New York, Nicolas Maduro alitarajiwa kufika mbele ya jaji leo umatatu saa sita mchana saa za huko Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili jioni Donald Trump alibainisha kwamba Marekani sasa “inaiongoza” Venezuela. Akiagizwa kufuata matakwa ya Washington, Delcy Rodríguez, aliyeteuliwa kuwa kaimu rais na Mahakama Kuu ya nchi yake, alionyesha nia yake ya kushirikiana na Washington ndani ya mfumo wa “uhusiano wenye usawa na heshima (…) unaotegemea usawa wa uhuru na kutoingiliwa.”

Takriban Wacuba 32 waliuawa wakati wa operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela iliyosababisha kukamatwa kwa rais Nicolas Maduro, Havana ilitangaza siku ya Jumapili. Wanajeshi waliouawa, wote wakiwa wanachama wa Kikosi cha Wanajeshi wa Mapinduzi au wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Cuba, walikuwa wakifanya katika ujumbe nchini Venezuela “kwa ombi la vyombo vya wenzao” katika nchi hiyo, ambayo ni mshirika wa karibu wa kisiwa hiki cha kikomunisti, serikali ya Cuba ilisema, ikitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.

Naye Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema leo Jumatatu wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri kwamba “njia iliyotumiwa” na Marekani kumkamata rais wa Venezuela Nicolas Maduro “haikuungwa mkono wala kuidhinishwa” na Ufaransa, msemaji wa serikali amesema, akiongeza kwamba Maduro alikuwa “dikteta” na kwamba kuondoka kwake ilikuwa “habari njema kwa Wavenezuela.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *