/

Chanzo cha picha, Donald Trump / Truth Social

    • Author, Gareth Evans
    • Akiripoti kutoka, Washington
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Kwa miezi kadhaa, majasusi wa Marekani walikuwa wakifuatilia kila hatua na nyendo za Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

Kilikuwa ni kikundi kidogo cha majasusi, kilichofanya kazi pamoja na chanzo kimoja cha ndani ya serikali ya Venezuela. Walimfuatilia Maduro mwenye miaka 63 kwa kila hatua, walijua wapi analala, anakula nini, anavaa nguo gani na kwamujibu maafisa wa juu wa jeshi, waliwajua hadi “wanyama wake pendwa aliowafuga” nyumbani.

Sasa baada ya kukusanya taarifa zote hizo za kijasusi, kilichofuata kikawa ni kukamilisha mpango wa kumkamata. Hilo lilitekelezwa mwanzoni mwa mwezi Disemba 2025, operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la “Absolute Resolve” ilisukwa kwa umakini mkubwa.

Hatua hiyo ilikuwa ni matokeo ya miezi ya kujipanga na mazoezi ya kijeshi ya kina, ambayo hyalijumuisha wanajeshi wa vikosi maalumu.

Wanajeshi hao walitengeneza mpaka nyumba iliyofanana kabisa na nyumba yenye ulinzi mkali ambayo Maduro alikuwa akiishi Caracas ili kufanya mazoezi ya namna watakavyiovamia, kumkamata na kuondoka naye.

Oparesheni hiyo – ambayo ni kubwa zaidi Marekani kuitekeleza Amerika ya Kusini ambao tangu enzi za Vita Baridi – ilisukwa kwa usiri mkubwa. Bunge la Congress la Marekani halikufahamishwa au kuombwa ushauri.

Toka Disemba mwanzoni, wakuu wa jeshi la Marekani pamoja na majasusi wao walisubiri wakati na mazingira muafaka wa kutekeleza shambulio hilo. Trump aliwapa ruhusa ya kushambulia siku nne kabla lakini walisubiri hali ya hewa itulie pamoja na mawingu mazito kuondoka.

‘Bahati nzuri na neema ya Mungu’

Usiku wa Ijumaa ulipofika amri ya mwisho ya uvamizi ikatoka, kilichofuata ilikuwa ni oparesheni iliyochukua saa mbili na dakika ishirini na kutekelezwa kutokea angani, ardhini na baharini.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, zaidi ya ndege 150 za kijeshi – zenye uwezo wa kipelelezi, kuangusha makombora makubwa na ndege vita zilitanda angani wakati wote wa operesheni.

Wakaazi wa Caracas waliamshwa na milio mikubwa ya milipuko kutoka angani saa nane za usiku, sawa na saa tatu asubuhi kwa Afrika Mashariki.

Wakati makombora ya Marekani yakiendelea kulenga maeneo mbalimbali ya kijeshi ya Venezuela ili kuzuia jeshi kuzima mashambulizi ya Marekani, makomando wa kikosi maalumu cha Delta Force walivamia makazi ya Maduro na kumteka na kuondoka naye baada ya kukabiliana na walinzi wake.

Trump akawa wa kwanza kuthibitisha shambulio hilo na kukamatwa kwa Maduro na mkewe ambao waliondolewa Venezuela kwa helikopta, kisha kusafirishwa kwa meli ya kivita na hatimaye ndege mpaka New York ambapo wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka.

Trump hakufuatilia did not follow the mission from the White House situation room. Trump alishuhudia uvamizi huo mubashara katika kasri lake la Mar-a-Lago alisema: ”lilikuwa jambo la kuvutia kuliona, na kuwa ilikuwa kama anatazama filamu.

Wengine waliyekuwa pamoja naye kufuatilia tukio ni Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio.


Picha inaonyesha Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Rais Donald Trump na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

Kutoka kushoto: Waziri wa ulinzi Pete Hegseth, CMkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Rubio na Trump

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

A photograph posted by U.S. President Donald Trump on his Truth Social account shows U.S. Secretary of Defense Pete Hegseth sitting next to Chairman of the Joint Chiefs of Staff Dan Caine as CIA Director John Ratcliffe stands next to a screen showing posts on the X.com website

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

Katika miezi ya hivi karibuni, maelfu ya wanajeshi wa Marekani walipelekwa katika eneo hilo, kujiunga na meli za kubeba na ndege na makumi ya meli za kivita katika operesheni kubwa zaidi kijeshi katika miongo kadhaa huku Trump akimshutumu Maduro kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na ugaidi, na kulipua makumi ya boti ndogo zinazotuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya katika eneo hilo.

Lakini dalili za kwanza za Operesheni zilikuwa angani. Zaidi ya ndege 150 – ikiwa ni pamoja na ndege za kudondosha makombora, ndege za kivita na ndege za upelelezi – hatimaye zilitumwa usiku kucha, kulingana na maafisa wa Marekani.

“Ilikuwa shughuli pevu, ngumu sana, maarifa kama yote, kutua, idadi ya ndege,” Trump aliambia Fox News. “Tulikuwa na ndege za kivita tayari kukabiliana na hali yoyote.”

Milipuko mikubwa ilisikika mjini Caracas mwendo wa saa nane usiku saa za ndani (06:00 GMT), na moshi mwingi ulionekana ukufuka juu ya jiji. “Nilisikia sauti kubwa, kishindo kikubwa,” ripota Ana Vanessa Herrero aliambia BBC. “Ilifunga madirisha yote. Mara baada ya kuona wingu kubwa la moshi ambalo karibu limzuie kuona kinachoendelea.”

Aliongeza: “Ndege na helikopta zilikuwa zikipaa juu ya anga lote la katika jiji la Caracas.”