
Maria Corina Machado, kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, ametangaza siku ya Jumatatu kwamba anakusudia kuifanya nchi yake, ambayo ina akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani, “kitovu cha nishati” cha Amerika, siku mbili baada ya Marekani kumkamata Rais Nicolas Maduro.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tutaifanya Venezuela kuwa kitovu cha nishati cha Amerika, tutaleta utawala wa sheria, tutafungua masoko, tutahitaji usalama kwa uwekezaji wa kigeni,” mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2025 ameiambia Fox News. Anapanga kurudi Venezuela “haraka iwezekanavyo” hata kama Donald Trump hatamuunga mkono kuchukuwa mamlaka ya nchi hiyo.
Wakati huo huo Nicolas Maduro amefika mbele ya jaji wa Marekani siku ya Jumatatu, Januari 5, katika kikao ambapo mashtaka dhidi yake nchini Marekani yametangazwa rasmi.
Nicolas Maduro amekana hatia mbele ya mahakama ya New York siku ya Jumatatu. Atabaki gerezani hadi kikao chake kijacho, kilichopangwa kufanyika Machi 17. “Mimi bado ni rais wa nchi yangu,” ametangaza wakati akisikilizwa mbele ya mahakama.
Venezuela imewaamuru polisi kumtafuta na kumkamata mtu yeyote aliyehusika na shambulio la Marekani. Spika wa Bunge la ameahidi kutumia “taratibu zote zinazowezekana” kwa ajili ya kurejea kwa Nicolas Maduro.
Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa anataka kuheshimiwa kwa “uhuru wa kisiasa” wa mataifa.
Milio ya risasi imeripotiwa karibu na ikulu ya rais huko Caracas siku ya Jumatatu jioni. Mamlaka inasema hali imedhibitiwa.
Baada ya kutetea uhusiano wenye usawa na heshima na Washington wakati wa mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri Jumapili, Delcy Rodriguez aliapishwa rasmi kama rais wa mpito wa Venezuela huko Caracas.