Rais wa Kongo amzuru Luanda, Angola, mnamo Januari 5, 2026. Nchini Angola,rais Felix Tshisekedi amekutana na mwenzake, João Lourenço, mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU). Wakuu hao wawili wa nchi walijadili hasa hali ya mashariki mwa DRC, eneo ambalo linakabiliwa na mzozo kati ya kundi lenye silaha la AFC/M23, linaloungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda, na vikosi vya Kongo na washirika wao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi

Rais wa DRC alifanya safari fupi, akiondoka Kinshasa yapata saa 11:00 alfajiri Jumatatu kuelekea Luanda. Alitumia saa chache na mwenzake wa Angola kabla ya kurudi nyumbani alasiri. Kulingana na Félix Tshisekedi, ziara hiyo ni kwa ajili ya jitihada za rais wa Angola. Katikati ya mkutano huu: mgogoro wa usalama mashariki, hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Kulingana na Félix Tshisekedi, João Lourenço alimpa mapendekezo ambayo aliyaona kuwa “ya kuvutia sana” katika kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo huo. Hata hivyo, mkuu wa nchi wa Kongo amebainisha kwamba hali iliyopo ni “ya vita ambayo imetukabili.”

Mshirika wa Kinshasa

Angola ni mmoja wa washirika wa Kinshasa katika mgogoro huu mashariki mwa DRC. João Lourenço alihusika sana katika mchakato wa Luanda, ambao ulikusudiwa kuanzisha uhusiano kati ya DRC na Rwanda.

Kwa hivyo, Félix Tshisekedi husafiri mara kwa mara hadi nchi hii inayozungumza Kireno, jirani wa DRC. Alikuwepo mwishoni mwa mwezi Novemba kwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya na tena katikati ya mwezi Desemba kwa ziara ya pande mbili.

João Lourenço pia ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, nafasi ambayo anatarajiwa kuikabidhi Burundi katika mkutano ujao wa shirika hilo katika mwezi mmoja. Burundi pia ni mshirika wa DRC katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *