
Thailand imeishutumu Cambodia siku ya Jumanne, Januari 6, kwa kukiuka usitishaji mapigano wao, ambao ulikuwa umeanza kwa siku 10, kwa urushaji wa makombora yaliyomjeruhi mmoja wa wanajeshi wake katika eneo la mpakani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Cambodia imekiuka usitishaji mapigano,” jeshi la Thailand limesema katika taarifa. “Vikosi vya Cambodia vimerusha makombora katika eneo la Chong Bok. Mwanajeshi mmoja amejeruhiwa na vipande vya makombora.”
Kambodia haikujibu mara moja shutuma hiyo.
Usitishaji mapigano ulimaliza mapigano ya wiki tatu mnamo Desemba 27, ambayo yalisababisha vifo vya watu wasiopungua 47 na kusababisha karibu watu milioni moja kutoka pande zote mbili za mpaka unaozozaniwa kutoroka makazi yao.