
Machado ameiambia televisheni ya Marekani ya Fox News kuwa Januari 3 itakumbukwa katika historia kama siku ambayo haki iliuangusha udhalimu. Machado hapo awali alikuwa amemsifu Trump kwa mtazamo wake mkali kuelekea Venezuela.
Baada ya kukamatwa kwa Maduro, Machado ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, alitoa wito kwa mwanasiasa wa upinzani Edmundo González Urrutia kuteuliwa kuwa rais. Mwanadiplomasia huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 76 alizingatiwa na wapinzani na waangalizi wa kimataifa kuwa alishinda kura ya urais mwaka wa 2024, ambayo iligubikwa na madai ya ulaghai. Aligombea tu kwa sababu Machado ambaye ni maarufu zaidi alikuwa amefungiwa kushiriki.
Hivi majuzi Trump alidokeza kwamba Machado hatachukua jukumu la kuiongoza Venezuela, akisema: “Itakuwa vigumu sana kwake kuwa kiongozi wa nchi kwa sababu hana uungwaji mkono au heshima ndani ya nchi.”
Makamu wa Rais wa Maduro Delcy RodrĂguez aliapishwa kama kaimu rais. Serikali yake inaendelea kumchukulia Maduro kama kiongozi halali wa nchi.