Takwimu hizi zinajumuisha vifo vya watu wengine 9 waliofariki dunia katika jimbo la mashariki mwa Rwanda wiki hii baada ya kupigwa na radi wakiwa njiani kutoka shambani.
Mkasa huu wa watu 9 waliopigwa na radi na kufarikidunia papo hapo ulitokea katika jimbo la mashariki mwa Rwanda wiki hii na watu wengine kumi na watano walijeruhiwa vibaya .
Huu pia ni ushahidi kwamba kile taasisi za kimataifa na hata mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Rwanda zimekuwa zikisema kwamba badhi ya maeneo ni hatari hasa wakati wa mvua za masika. Kwa sasa manusura wa mkasa huo wa radi wanaendelea kupewa matibabu katika hospitali mbalimbali za jimbo la mashariki na miili ya walioufa imeshazikwa na jamaa zao kwa msaada wa serikali.
Tukio hilo lilitokea wakati ambapo wananchi hao walikuwa njiani kurejea nyumbani kutoka shambani mvua iliponyesha na kusababisha radi hiyo. Haikuwezekana kuzungumza moja kwa moja na manusura lakini naibu mkuu wa wilaya ya Ngoma upande wa mashariki mwa Rwanda kulikotokea mkasa huo Jean De Dieu Ndaruhutse amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa picha ya tukio lenyewe lakini pia akazungumzia wale walioko hospitali.
“Ni wananchi waliokwenda kulima katika bonde la Jarama, lakini baadaye walipokuwa wakiejea nyumbani mvua ilinyesha na wao kujesitiri katika nyumba ndogo iliyokuwa pembeni mwa njia ambapo radi iliwapiga na 9 kati yao wakafariki dunia,lakini kikubwa ambacho sasa tunafanya kama serikali ni kuwapa faraja manusura na wananchi kwa ujumla lakini tukirejelea ile kauli ule mwito wetu wa awali kwamba wananchi waendelea kuwa makini wakati wa mvua. Tunasema mvua ikinyesha watu waepuke kutumia vyombo vya umeme kama vile kuzungumza kwa simu,usikae chini ya mti wakati mvua ikinyesha lakini pia epuka kufungua redio au kuwasha vyombo vya umeme kwa ujumla.”
Mmoja wa wananchi aliyeshuhudia tukio hilo ameonyesha wasi wasi wa angalizo hilo akisema hali hii inaendelea kuweka taharuki miongoni mwa wananchi hasa wakati huu mvua za masika zinapotarajia kuanza kunyesha mwezi wa nne. Hata hivyo kutokana na kwamba hakutaka kutajwa jina amesema ma nyingi mamlaka zinalishughulikia tatizo hili pale yanapopotea maisha ya watu na baadaye mamlaka zinaendelea na mambo mengine.
Kutokana na hali ya miinuko na mabonde mengi Rwanda imekuwa ikikabiliwa kwa kiasi kikubwa na athari za mafuriko, maporomoko ya milima na hata kupoteza maisha ya wananchi. Wakati mvua zikianza licha ya tatizo la radi katika baadhi ya sehemu za wizara inayoshughulikia majanga hutoa angalizo kwa wananchi kuwa makini na ikiwezekana kuondoka katika maeneo hatarishi. Bi Niyotwambaza Christine ameiambia televisheni ya taifa hatua zinazochukuliwa kuweka tahadhari kwa wananchi zinatokana na utabiri wa hali ya hewa
“Tunaposhikirikiana na mamlaka ya hali ya hewa nchini,inatusaidia kujua ni wapi hasa tunapaswa kuweka nguvu na umakini mkubwa hasa kwa sasa tunapotegemea kuingia katika msimu wa masika, kwa sasa tunajiandaa kuweka juhudi za kukabiliana na upepo mkali na radi ambayo inachukua uhai wa watu wetu, lakiini pia upepo unaharibu miundo mbinu kwa kiezua mapaa ya shule zetu.”
Licha ya juhudi zinazoendelea kuwataka wananchi kuwa makini na kuyahama maeneo hatarishi wadadisi wanahisi kuwa kusuasua katika kufuatilia utekelezwaji wa agizo hili haujaleta tija inayotakiwa.
