Kiongozi wa kijeshi wa Iran alionya kwamba Iran haitakaa kimya, baada ya Marekani na Israel kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali.

“Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inachukulia kuongezeka kwa kauli za uhasama dhidi ya taifa la Iran kuwa tishio na haitavumilia kuendelea kwake bila kujibu,” alisema Jenerali Amir Hatami, kwa mujibu wa shirika la habari la Fars siku ya Jumatano.

Hatami, kamanda wa jeshi la Iran, alionya kwamba “ikiwa adui atafanya kosa” mwitikio wa Iran utakuwa mkali zaidi kuliko ule wa wakati wa vita vya siku 12 dhidi ya Israel mwezi Juni 2025.

Hivi karibuni, Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuingilia kati iwapo Iran itauwa waandamanaji, wakati huo huo Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel ameonyesha kuunga mkono maandamano hayo.

Tarehe 28 Disemba wafanyabiashara mjini Tehran walifanya maandamano kupinga ongezeko la bei na kuanguka kwa sarafu ya nchi hiyo rial, jambo lililosababisha maandamano kama hayo kufanyika katika miji kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *