Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umefanya mashambulizi ya anga katika mkoa wa  nyumbani kwa kiongozi wa waasi wanaoungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, nchini Yemen, Aidaros al-Zubaidi, baada ya kiongozi huyo kushindwa kufika Riyadh kwa mazungumzo. 

Yemen

Muungano huo ulisema ulimpa al-Zubaidi muda wa saa 48 afike Riyadh, kufuatia kundi lake la Barala la Mpito la Kusini, STC, kutwaa maeneo makubwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, al-Zubaidi hakupanda ndege iliyokuwa imebeba ujumbe wake, hatua iliyovisukuma vikosi vya muungano wa kijeshi kushambulia jimbo la al-Dhale, vikimtuhumu kuandaa vikosi vikubwa vya kijeshi.

Wahouthi waelekea Saudi Arabia kwa mazungumzo ya amani Yemen

Baadaye, Baraza la Uongozi wa Rais, PLC, likiongozwa na Rashad al-Alimi, lilitangaza kumvua al-Zubaidi wadhifa wake, likimtuhumu kwa uhaini, kudhoofisha jeshi na uchumi wa taifa, pamoja na kuunda kundi la wapiganaji.

Mvutano huu umeibua hofu kwamba mji wa Aden huenda ukatumbukia katika ghasia mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *