
Tangu mashambulizi ya Marekani usiku wa Ijumaa, Januari 2 kuamkia Jumamosi, Januari 3, na kutekwa nyara kwa Nicolas Maduro, mvutano umekuwa ukiongezeka nchini Venezuela, hasa kutokana na kupelekwa kwa makundi ya wanamgambo wanaounga mkono utawala katika mitaa ya Caracas.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hali ya hatari sasa inaanza kutumika, ikiruhusu kukamatwa kwa mwandamanaji yeyote anayesherehekea operesheni ya Marekani. Baada ya kukana hatia katika mahakama ya New York Jumatatu, Januari 5, Rais aliyeondolewa madarakani Nicolás Maduro na mkewe bado wako kizuizini nchini Marekani.
Nchini Venezuela, hali ya hatari (inayoitwa rasmi “hali ya machafuko ya nje”) imetangazwa, na makundi ya wanamgambo wenye silaha yamesambazwa katika mitaa ya Caracas ili kudumisha utulivu. Kulingana na sheria hii, mtu yoyote anayeounga mkono operesheni ya Marekani anaweza kukamatwa. Sheria hiyo ilipitishwa mnamo mwezi Septemba na rais anayeshikiliwa na Marekani, Nicolás Maduro.
Angalau watu wawili tayari wamekamatwa kwa kusherehekea kutekwa nyara kwa Nicolas Maduro, anaripoti mwandishi wetu huko Caracas, Alice Campaignolle.
Katika kitongoji cha Boleita, mashariki mwa Caracas, wanaume wenye silaha wamekuwa wakizunguka kwa siku kadhaa, kama ilivyoelezwa na mkazi huyu ambaye hakutaka jina lake litajwe. “Jana, niliwaona, na nikahesabu, walikuwa angalau 100. Na wakiwa na bunduki ndefu,” anasema. Vizuizi vya barabarani pia vimewekwa kwenye barabara kuu. Wanaume wanaojifunika nyuso zao huangalia vitambulisho, hukagua magari, na si hayo tu. “Wanaangalia kila kitu, hata simu yako. Mimi natambea simu ya zamani kila wakati, wakiihitaji ninawapa. Watu wanaogopa.” Na kwa amri hii waliyosaini, hali itakuwa mbaya zaidi. Wanaweza kukukamata bila hatia, bila sababu yoyote, bila kesi,” mtu huyo ameongeza.
Wakati mwingine kuna maafisa wa polisi, na watu wanawadhania kuwa wanamgambo. Naam, hata kama ni wanamgambo… Sitoki nje usiku, kwa hivyo sina cha kuogopa. Ninaenda kazini mchana tu, basi. Wale wanaobeba silaha ni dhahiri wanalinda nchi yetu.
Operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela: Je, Donald Trump alikiuka Katiba ya Marekani?
Tangu kukamatwa kwa Nicolas Maduro nchini Venezuela, upinzani katika Bunge (chama cha Democratic) unamshumu Donald Trump kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ya kikatiba, ukisema kwamba rais wa Marekani angepaswa kushauriana na kuarifu Bunge kabla ya kuanzisha shambulio nchini Venezuela.