Waziri wa mambo ya nje wa Uchina, Wang Yi, ameanza ziara rasmi barani Afrika ambapo atatembelea nchi kadhaa katika kile ofisi yake imesema ni kumarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa hayo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wang Yi, atazuru nchi za Ethiopia, Somalia, Tanzania na Lesotho, ziara ambayo wadadisi wa mambo wanasema ni Beijing kutaka kuimarisha mizizi ya ushirikiano wake na bara la Afrika hasa wakati huu Marekani na washirika wake wakijaribu kupunguza ushawishi wake kwenye bara hilo.

Ziara ya Wang Yi nchini Somalia inalenga kuonesha uungaji mkono wake kwa taifa hilo la pembe ya Afrika, ambapo wiki iliyopita kwenye baraza la usalama Beijing ilikashifu Israel kutambua Somaliland kama nchi huru.

Aidha ziara yake nchini Tanzania imekuja miezi kadhaa kupita tangu taifa hilo lishuhudie vurugu za baada ya uchaguzi wa Octoba mwaka jana, ambapo raia zaidi ya 500 wanadaiwa kuuawa na vyombo vya usalama.

Nchi ya China ni mshirika mkubwa wa kibiashara kwa bara la Afrika ambapo kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Beijing, nchi hiyo ilifanya biashara na bara hilo inayofikia dola za Marekani bilioni 296 mwaka 2024, China ikituma maelfu ya raia wake kufanya kazi kwenye barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *