Mali ilicheza wakiwa pungufu baada ya beki Woyo Coulibaly kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 26, lakini walimudu na kulazimisha sare ya 1–1 na hatimaye kusonga mbele kwa mikwaju ya penalti.

Kiungo Lassana Coulibaly amesema ushindi dhidi ya Tunisia ulitokana na nguvu ya kisaikolojia, akisisitiza kuwa watahitaji uimara huo huo watakapokutana na Senegal siku Ijumaa.

Mali wanasema hawana cha kupoteza, ingawa Senegal—wanaoshika nafasi ya pili barani Afrika na tayari wakiwa na mabao 10 kwenye mashindano haya wanaonekana kuwa miongoni mwa wagombea wakuu wa kutinga nusu fainali.

Kocha wa Mali, Tom Saintfiet, amesema Senegal ni timu thabiti na hatari, ikizingatiwa kuwa katika miaka ya karibuni wamepoteza mechi moja tu dhidi ya Brazil. Hata hivyo, amesisitiza kuwa Mali pia ni timu imara, haijapoteza mchezo wowote kwenye mashindano haya na imeonyesha ubora dhidi ya Morocco na Tunisia.

Hii ni mara nyingine kwao kujaribu kuvunja nuksi, kwani hawajawahi kutwaa taji la AFCON tangu walipokuwa washindi wa pili mwaka 1972, na kufika nusu fainali mara tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *