Nchini Cote Dvoire, Waziri Mkuu Robert Beugré Mambé na serikali yake imejiuzulu, baada ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Desemba 27 mwaka uliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Allasane Ouattara siku ya Jumatano, alikubali kujiuzulu kwa Mawaziri wake na Waziri Mkuu Mambé, licha ya chama chake cha RHDP kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 77.

Hatua hii pia inakuja, miezi miwili baada ya rais Ouattara kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, baada ya kupata ushindi wa karibu asilimia 90 ya kura.

Rais Outtara sasa anatarajiwa kumtaja Waziri Mkuu mpya na kuwateuwa Mawaziri wapya katika siku zijazo, baada ya chama chake kupata viti 198 kati ya 255 katika bunge la kitaifa.

Ripoti zinasema, huenda baadhi ya Mawaziri waliojizulu wakarejeshwa tena kwa sababu, wamechaguliwa kama wabunge.

Licha ya kujiuzulu, kiongozi wa nchi hiyo, amewaomba Waziri hao kuendelea kusimamia shughuli katika wizara mbalimbali hadi pale warithi wao watakapoteuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *