
Hali inazidi kuwa mbaya katika katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC. Kundi la waasi la CRP, kundi linaloongozwa na Thomas Lubanga – mfungwa wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu- linagonga vichwa vya habari tena. Ingawa kundi hilo lilionekana kudhoofika baada ya operesheni za jeshi la Kongo, mapigano mapya yalishhudiwa katika wiki za hivi karibuni. Takwimu za awali zinaanza kujitokeza.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati umakini ukiendelea kulenga mkoa wa Kivu Kaskazini, hali ya usalama inaendelea kuwa ya kutia wasiwasi sana katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mapema mwaka wa 2015, Thomas Lubanga, ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Uganda, alianzisha harakati za kisiasa na kijeshi: Mkataba wa Mapinduzi ya Kiraia (CRP).
Anasema anafanya kazi kwa hasira dhidi ya serikali ya Kinshasa, ambayo anaishutumu kwa kuipora Ituri na kupuuzia mkoa huo, haswa kwa kupendelea migogoro ya usalama huko Kivu. Tangu wakati huo, CRP imekuwa mojawapo ya makundi yaliyo hai zaidi na yanayotajwa mara kwa mara huko Ituri.
Wapiganaji wake walionekana katika wiki za hivi karibuni karibu na Bule, mji ulioko takriban kilomita 95 kutoka Bunia, mji mkuu wa mkoa. Kitovu hiki cha kibiashara hutekwa mara na vikosi vya jeshi la setikali, mara na makundi ya waasi, wakati mapigano yakiendelea: wakati mwingine hukaliwa na CRP, wakati mwingine huchukuliwa tena na jeshi la Kongo. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika siku za hivi karibuni.
Kulingana na ripoti za hivi karibuni, Bule inadhibitiwa tangu siku ya Jumatano, Januari 7, 2026, na wanamgambo wanaoshutumiwa na jeshi kwa kutumia watu waliokimbia makazi yao na raia wengine kama ngao za binadamu.
Na idadi ya waathiriwa ni kubwa. Kulingana na vyanzo vya Umoja wa Mataifa, angalau raia 25 waliuawa na zaidi ya 40 walijeruhiwa katika mwezi uliopita huko Bule na maeneo ya jirani.
Tangu Desemba 26, watu 23 waliojeruhiwa vibaya wamehamishiwa Hospitali Salama huko Bunia, kituo kinachoungwa mkono na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (RSF).
Katika Hospitali ya Fataki, iliyoko takriban kilomita 15 kutoka Bule, watu 22 waliojeruhiwa pia wametibiwa.
Hali ya kibinadamu ni mbaya. Kulingana na OCHA, ukosefu wa usalama unazuia upatikanaji wa misaada kwa zaidi ya watu 87,000 waliokimbia makazi yao ndani na karibu na Bule.
Mamlaka katika eneo hilo pia zinaripoti kwamba angalau watu 17 walifariki kati ya Desemba 5 na 29 kutokana na hali ngumu ya maisha, ukosefu wa huduma za matibabu na njaa.