Wakati mkutano wa kilele wa mawaziri wa ulinzi kutoka eneo la Maziwa Makuu ukifunguliwa nchini Zambia siku ya Alhamisi, Januari 8, sherehe ilifanyika siku hiyo hiyo mashariki mwa DRC kuwaenzi wahanga sita wa mlipuko uliotokea Januari 2 katika mji wa Masisi-centre. Chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana, na kuibua maswali mengi kuhusu kusitisha mapigano. MONUSCO imetoa wito wa uchunguzi huru na kuanzishwa kwa uwajibikaji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa saa 7 usiku mnamo Januari 2 huko mkini kati Masisi, mji ulioko katika mkoa w Kivu Kaskazini kwa sasa uko chini ya udhibiti wa M23. Wakazi wengi waliohojiwa walielezea mlipuko kutoka angani, “sauti kama ya kombora,” walisema, ikifuatiwa na mlipuko mkali.

Nyumba kadhaa zilikumbwa na shambulio hilo, karibu na jengo kunakopatikana ofisi ya mkuu wa eneo la Masisi. Jengo la shirika lisilo la kiserikali la War Child pia lilipigwa. Paa lilidondoka.

Watu wanne walifariki katika eneo la tukio, na majeruhi 43 walipelekwa Hospitali ya Masisi. Wawili kati ya waliojeruhiwa baadaye walifariki kutokana na majeraha yao, na wanne walihitaji upasuaji mkubwa.

Shambulio la ndege zisizo na rubani?

Shambulio la ndege zisizo na rubani? Hakika hiyo ndiyo dhana inayotolewa. Lakini ilitoka wapi? Na zaidi ya yote, ni nani anayehusika?

Kwa AFC/M23, hakuna shaka: shambulizi hilo lilifanywa na jeshi la Kongo. Kundi hili la waas limeandaa sherehe huko Goma siku ya Alhamisi, Januari 8, ili kuwaenzi waathiriwa.

Kwa upande wake, MONUSCO, katika taarifa iliyotolewa Januari 3 kwenye mtandao wa kijamii wa  X, ilitoa wito wa uchunguzi huru wa kitendo hiki na mhusika kuwajibishwa.

Mnamo mwezi Machi 2025, miezi kumi mapema, mashambulizi mengine mawili yalilenga kilima kimoja karibu na jiji hili.

Ni katika muktadha huu ambapo mkutano wa maafisa wa kijeshi na mawaziri wa ulinzi kutoka eneo la Maziwa Makuu ulifunguliwa siku ya Alhamisi, Januari 8, nchini Zambia. Lengo: kujaribu kufufua utaratibu wa ufuatiliaji na utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa kati ya Kinshasa na AFC/M23, na kati ya Kinshasa na Kigali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *