Jeshi limetangaza amri ya kutotoka nje katika maeneo ya Sheikh Maqsoud na Ashrafieh na kuwataka wakazi wahame mara moja, likisema litalenga maeneo yanayodaiwa kutumiwa na wapiganaji wa SDF. Maelfu ya raia tayari wamekimbia makazi yao, huku vifo na majeruhi vikiripotiwa.

SDF imesema inapambana na makundi yanayoiunga mkono Damascus karibu na kitongoji kinachokaliwa na Wasyria na kudai kuwa imewasababishia hasara kubwa.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Kikurdi ya Iraq, Masrour Barzani, ameeleza wasiwasi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya vitongoji vya Wakurdi, akionya kuwa yanaweza kufikia kiwango cha maangamizi ya kikabila.

Akizungumzia mapigano hayo, Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema “Umoja wa Mataifa unasisitiza tena kwamba pande zote zina wajibu wa wazi, chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu, kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia. Tunatoa wito kwa wahusika wote kupunguza mvutano mara moja, kuwa na kiwango cha juu cha kujizuia, na kuchukua hatua zote zinazohitajika kuzuia madhara zaidi kwa raia.

Dujarric amehimiza pande zote kuonyesha ustahimilivu na nia njema, kijeshi na kisiasa, na kurejea mara moja kwenye mazungumzo ili kutekeleza kikamilifu makubaliano ya Machi 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *