Hii ni  baada ya vuguvugu lake la Baraza la Mpito la Kusini (STC), linaloungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, kujaribu kuyateka maeneo mengi na kisha kujitangazia uhuru katika eneo la Kusini mwa Yemen.

Alzubidi aliyeshutumiwa kwa makosa ya uhaini, aliondolewa katika Baraza la Uongozi la Rais wa Yemen siku ya Jumatano, na wakati huo huo muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulishambulia kwa mabomu mkoa wake wa Kusini baada ya yeye kushindwa kufika mjini Riyadh kuhudhuria mazungumzo.

Umoja wa Falme za Kiarabu haujatoa tamko lolote mpaka sasa.

Mashambulizi ya STC ya mwezi uliopita yalileta msukosuko mpya katika nchi ya Yemen iliyogawanyika, na kufichua migawanyiko mikubwa kati ya washirika wa Ghuba, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *