Kulingana na Rais wa Marekani Donald Trump, udhibiti wa Marekani kwa Venezuela unaweza kudumu “muda mrefu zaidi” kuliko mwaka mmoja, amesema katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya Alhamisi, Januari 8, na Gazeti la New York Times.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Marekani inaweza kudumisha udhibiti wa Venezuela kwa miaka kadhaa, amesema Rais wa Marekani Donald Trump katika mahojiano yaliyochapishwa Alhamisi, Januari 8, na Gazeti la New York Times.

Katika mahojiano ya saa mbili na gazeti hilo, rais Donald Trump ametangaza kwamba hajui ni muda gani upelelzi na ukaguzi kwa nchi hiyo ya Amerika Kusini utadumu. “Tusibiri tuone jinsi hali itakavyokuwa,” amejibu, saa chache baada ya maafisa wa utawala kusema kwamba Marekani imepanga kuchukua udhibiti wa mauzo ya mafuta ya Venezuela “kwa muda usiojulikana.”

Alipoulizwa kama hali hiyo ingedumu kwa miezi mitatu, miezi sita, mwaka, au zaidi, Donald Trump amejibu: “Ningesema muda mrefu zaidi.” “Tutajenga upya nchi hiyo kwa njia yenye gharama nafuu sana,” rais wa Marekani ameongeza. “Tutatumia mafuta na kuyaagiza kutoka nje. Tutapunguza bei ya mafuta na kutoa pesa kwa Venezuela, ambayo inaihitaji sana,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *