Waziri anayehusika na Huduma za Dharura, Oleksiy Kuleba amesema watu wanateseka katika kipindi hiki cha baridi kali sawa na ilivyokuwa katika majira ya baridi ya mwaka uliopita. 

Waziri huyo amesema kazi ya ukarabati inaendelea katika eneo hilo la Dnipropetrovsk ili kurejesha umeme na maji.

Mkazi mmoja wa eneo lililoathiriwa anaeleza “Umeme ulikatika usiku, tulihisi usumbufu mkubwa. Jambo baya ni kwamba vifaa vya kutia joto majumbani havifanyi kazi, baridi ni kali sana na hatujui tutajiokoa vipi.”

Urusi imeongeza mashambulizi yake katika miundombinu ya nishati ya Ukraine, ambapo eneo la Zaporizhzhia pia lilishambuliwa na kusababisha kukatika kwa umeme na maji. Serikali ya Ukraine na washirika wake imekitaja kitendo hicho kuwa ni mkakati wa makusudi wa Urusi unaowalenga raia moja kwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *