Zambia inajiandaa kuandaa mkutano mkubwa wa usalama katika eneo la Maziwa Makuu ambao umepangwa kufanyika Januari 10 wenye lengo hasa la kushughulikia changamoto za usalama katika kanda wa maziwa mamkuu, ambapo waaalamu wa usalama wa ICGLR wameanza kukutana leo huko Livingston nchini Zambia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kimsingi, mkutano huu ungeweza kufanyika nchini DRC ambayo kwa sasa ndiye mwenyekiti wa ICGLR. Lakini pia ndiyo nchi iliyoathiriwa moja kwa moja na ghasia katika eneo hilo.  

Kuna kipengele kingine muhimu.

Katika Mkutano wa mwisho wa ICGLR mjini Kinshasa, Rwanda haikuwakilishwa. Wakati huu, kuchaguwa ufanyike Livingstone, Zambia, kunalenga waziwazi kuunda mazingira yanayozingatiwa kuwa ya kutoegemea upande wowote.

Kiini cha mkutano huu ni utekelezaji madhubuti wa michakato ya Washington na Doha, haswa kipengele chao cha kusitisha mapigano. Huko Doha, Kinshasa na AFC/M23 zilitia saini utaratibu wa ufuatiliaji wa kusitisha mapigano.

Lakini kimsingi, itifaki hii haiheshimiwi. Moja ya sababu kuu ni kwamba utaratibu wa uthibitishaji na ufuatiliaji bado haufanyi kazi.

Utaratibu huu unategemea hasa Utaratibu wa Uthibitishaji wa Pamoja wa ICGLR (EJVM). Utaratibu huo pia ulijadiliwa huko Washington.

Katika hali halisi, hii ina maana kwamba ICGLR ndiyo kiini cha utekelezaji wa michakato hii miwili ya amani. Shida ni kwamba EJVM inafanya kazi kwa uwezo uliopunguzwa.

Inahitaji kuhuishwa ili kuruhusu ufuatiliaji unaofaa wa usitishaji mapigano. Na katika ufufuaji huu, Zambia inatarajiwa kuwa na jukumu muhimu. Kwa mujibu wa taarifa zetu, imeamuliwa kuwa kamanda mpya wa EJVM ya ICGLR atakuwa Mzambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *