Kutunza mapacha kunaweza kuwa changamoto, “hasa ​​katika miezi ya mwanzo wakati watoto wanategemea matunzo ya mama yao,” taarifa ya Hifadhi hiyo ilisema.

Iliongeza kusema kuwa watoto wachanga wanaangaliwa kwa karibu ili kuhakikisha wanakuwa.

Picha zilizotolewa na Shirika la Habari la Hifadhi hiyo zilimuonyesha Mafuko mwenye umri wa miaka 22 akiwa amewakumbatia watoto wake.

Mafuko alizaliwa katika familia ya Kabirizi lakini alijiunga na familia ya Bageni miaka sita baada ya mama yake kuuawa na “watu wenye silaha” mwaka 2007, taarifa ya hifadhi hiyo ilisema.

“Kuzaliwa kwa mapacha hawa kunawakilisha tukio kubwa kwa mienendo ya familia ya Bageni na kwa juhudi zinazoendelea za uhifadhi kusaidia ukuaji wa sokwe wa milimani walio hatarini kutoweka ndani ya Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa jumla, Mafuko sasa amezaa watoto saba, wakiwemo mapacha waliofariki wiki moja baada ya kuzaliwa mwaka 2016.

Familia ya Bageni sasa ina sokwe 59 na ndiyo kubwa zaidi katika hifadhi hiyo, ilisema taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *