Urusi imemwachilia huru mtafiti wa Ufaransa Laurent Vinatier kwa kubadilishana na kuachiliwa huru kwa mchezaji wa mpira wa kikapu wa Urusi Daniil Kasatkin, shirika la habari la Urusi TASS limeripoti leo Alhamisi, Januari 8, likinukuu Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB).

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyonukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi, FSB imedai kwamba Daniil Kasatkin amerudi Urusi siku ya Alhamisi na “alibadilishwa” kwa Laurent Vinatier. Alikamatwa mnamo mwezi Juni 2024, mtafiti huyo mwenye umri wa miaka 49 alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mnamo mwezi Oktoba mwaka huo kwa kushindwa kujiandikisha kama “afisa wa kigeni.” Alikuwa akikabiliwa na shtaka jipya la ujasusi tangu mwezi Agosti mwaka uliyopita.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imethibitisha kurudi kwa mtafiti huyo nchini Ufaransa na kwamba alipokelewa katika Quai d’Orsay (Wizara ya Mambo ya Nje).

Ufaransa imebainisha kwamba Laurent Vinatier  alikamatwa kiholela na ilioma maa kadhaa aachiliwe huru.

(Taarifa zaidi zitakujia)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *