Urusi imeiita Ukraine na Washirika wake nchi za Ulaya kama “wachochezi wa vita”, ikionya kuwa makubaliano waliyoafikiana jijini Paris kutuma wanajeshi wa kulinda amani huko Kiev ni suala ambalo Moscow haiwezi kukubali ili kumaliza vita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika maoni yake ya kwanza baada ya washirika wa Ukraine kukubaliana kuhusu dhamana muhimu za usalama kwa Kyiv, Urusi imekosoa mpango huo “wa kijeshi”, ikisisitiza kuwa hauna nia njema katika kumaliza vita inayoingia mwaka wa nne.

Viongozi wa Ulaya na wale wa Marekani walitangaza mapema wiki hii kwamba dhamana za usalama kwa Kyiv zitajumuisha utaratibu wa ufuatiliaji unaoongozwa na Marekani pamoja na kikosi cha kimataifa cha Ulaya ambacho kitatumwa ikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano yatafikiwa.

Washirika wa Ukraine walikutana wiki hii jijini Paris kujadili usalama wa Kyiv
Washirika wa Ukraine walikutana wiki hii jijini Paris kujadili usalama wa Kyiv © Ludovic Marin / via Reuters

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi, Maria Zakharova, katika taarifa yake amesema kuwa vifaa na askari wowote watakaotumwa Ukraine watahesabika na nchi yake kama shabaha halali za kijeshi.

Moscow imeonya mara kwa mara kwamba haitakubali mwanachama yoyote wa NATO kutuma wanajeshi wa kulinda amani nchini Ukraine, ikiwataja washirika hao wa Ukraine kama wachochezi na wanaotaka kuona vita ikiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *