Baada ya kumteka nyara na kumkamata rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Marekani imesema kwamba itadhibiti uzalishaji wa mafuta nchini humo na “kufufua” uwezo wa nchi hiyo wa kuzalisha mafuta.Kauli hii imeibua mjadala kuhusu umuhimu wa mafuta katika siasa za kimataifa. 

Rasilimali hii ya mafuta, Afrika pia imejaaliwa kuwa nayo kwa wingi.Kwa jumla Afrika inaripotiwa kuwa na zaidi ya mapipa bilioni 125 ya mafuta yaliyothibitishwa.

Libya ikiwa inaongoza katika orodha hiyo ambapo inakadiriwa kuwa na takriban mapipa bilioni 48.36, hiki ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika.

Mwaka 2025, Libya ilizalisha wastani wa juu zaidi wa mafuta ghafi katika zaidi ya muongo mmoja, na kufikia takriban mapipa milioni 1.37 kwa siku.

Hili ni ongezeko kubwa kubwa kwa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. Kabla ya machafuko ya 2011 ambayo yalisababisha kupinduliwa na kuanguka kwa utawala wa Muamar Gaddafi na hatimae kuibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe- nchi hiyo ilikuwa ikizalisha wastani wa mapipa milioni 1.6 hadi milioni 1.7 kwa siku.

Lakini baadae uzalishaji ukapungua.

Pato la taifa la mafuta nalo likapungua hadi kufikia mapipa 20,000 kwa siku. 

Vizuizi vya makundi yenye silaha, ushindani wa kisiasa, na hujuma dhidi ya miundombinu vyote vilichangia.

Serikali inasema ufufuaji wa uzalishaji karibu miaka 15 baadaye umechangiwa na uimarishaji mpana wa maeneo muhimu ya mafuta, vituo vya usafirishaji nje, na vifaa vya uendeshaji chini ya usimamizi wa Shirika la Mafuta la Kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *