Wanajeshi wa majini nchini Marekani, wamezuia meli ya mafuta inayohusishwa na Venezuela Januari tarehe 7.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Meli hiyo iliyopewa jina la M Sophia, iliyowekewa vikwazo na Marekani, ilizuiwa, baada ya kubainika kuwa haikuwa ya taifa lolote.

Komandi ya Marekani imesema, wanajeshi wa Marekani, imeisindikiza meli hiyo kwenda Marekani kwa ajili ya utaratibu mwingine.

Shirika la Habari la Reuters, imethibitisha kuwa video ya meli hiyo ni halali. Tarehe ambayo video hiyo ilichukuliwa Januari 7.

Meli hiyo iliondoka kwenda Venezuela mapema mwezi Januari, ikiwa imebeba mafuta ikielekea China, kwa mujibu wa ripoti za watalaam wa masuala ya baharí.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *