
Katibu mkuu wa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen Abdulrahman Jalal al-Sebaihi, amesema kundi hilo na taasisi zake zitavunjwa kuanzia Ijumaa baada ya wiki kadhaa za machafuko katika maeneo ya kusini na siku moja baada ya kiongozi wake kukimbiliaUmoja wa Falme za Kiarabu.
Akizungumza kwenye televisheni ya Yemen, al-Sebaih alisema mkutano ulifanyika ili kutathmini matukio mabaya ya hivi karibuni katika majimbo ya Hadramout na al-Mahra na baada ya kukataa juhudi zote za kutuliza hali ya mambo.
Hata hivyo, katika ishara dhahiri ya mgawanyiko wa ndani, msemaji wa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen Anwar al-Tamimi aliandika kwenye mtandao wa X kwamba maamuzi yanayohusiana na baraza yanaweza kufanywa tu na baraza hilo kwa ukamilifu wake na chini ya rais wake.
Pia amesema baraza litaendelea na ushirikiano wake chanya na wenye kujenga na mipango yote ya kisiasa kwa njia ambayo itawawezesha watu wa kusini mwa Yemen kuamua mustakabali wao.”