Sokwe wa milimani, amezaa mapacha katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Virunga, Januari 7 Mashariki mwa DRC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa mbunga hiyo, unasema hatua hiyo ni muhimu wakati huu wanyama hao wakiwa katika hatari ya kutoweka.

Sokwe huyo aliyepewa jina Mafuko, anaelezwa kuwa yupo katika hali nzuri na wanawe.

Mafuko mwenye umri wa miaka 22, alizaliwa kutoka familia ya Kabirizi kabla ya kuhamishiwa katika familia ya Bageni, akiwa na umri wa miaka sita baada ya kuuawa kwa mama yake na watu wenye silaha mwaka 2007.

Kwa ujumla, sokwe huyo ana watoto saba, wakiwemo mapacha wengine waliofariki duania wakiwa na wiki moja mwaka 2016.
Kwa ujumla, sokwe huyo ana watoto saba, wakiwemo mapacha wengine waliofariki duania wakiwa na wiki moja mwaka 2016. via REUTERS – Virunga National Park

Kwa ujumla, sokwe huyo ana watoto saba, wakiwemo mapacha wengine waliofariki duania wakiwa na wiki moja mwaka 2016.

Mbunga ya Virunga ni kongwe barani Afrika yenye ukubwa wa kilomita za mraba 3,000 ina sokwe wengi wa milimani duniani, licha ya sehemu yake kudhibitiwa na makundi ya waasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *