Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema Ijumaa kwamba hatua zinazochukuliwa na vyombo vya usalama vya Iran kuyazima maandamano zimechupa mipaka.

Ameongeza kusema machafuko yoyote dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani hazikubaliki.

Kallas ameandika katika mtandao wa X akisema kufunga mtandao wa intaneti na kukandamiza maandamano kunaufichua utawala unaoogopa watu wake wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *