Nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan, amemfuta kazi Waziri wake wa usalama George Simbachawene, huku akifanya mabadiliko madogo kwenye Baraza lake la Mawaziri.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka, nafasi ya Simbachawene sasa imechukuliwa na Patrobas Katambi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusu uamuzi wa kumwondoa Simbachawene kwenye nafasi hiyo, ambayo amekuwa akiitumikia tangu baada ya uchaguzi uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka uliopita.

Simbachawene  ambaye alikuwa anasikika akiwahimiza polisi kusimamia sheria katika majukumu yao, alikuwa anasimamia Wizara hiyo nyeti, huku jeshi la polisi nchini humo likishtumiwa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji kipindi cha uchaguzi.

George Simbachawene alikuwa Waziri wa usalama wakati wa maandamano yaliotokea nchini Tanzania
George Simbachawene alikuwa Waziri wa usalama wakati wa maandamano yaliotokea nchini Tanzania REUTERS – Thomas Mukoya

Katika hatua nyingine, Profesa Palamagamba Kabudi, ameondolewa kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na sasa ameteuliwa kuwa Waziri wan chi, Ofisi ya rais Ikulu kazi maalum, huku nafasi ikichukuliwa na aliyekuwa naibu wake Paul Makonda.

Haya ni mabadiliko ya kwanza madogo, kufanywa na rais Samia ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi uliopita kwa kupata asilimia 98 ya kura, uchaguzi ambao wapinzani wake wakuu kama Tundu Lissu ambaye yupo jela anakoshtumiwa kwa tuhma za uhaini, hakushiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *