MAMLAKA ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata kilogamu 9,689 za dawa za kulevya, pikipiki 11 na magari matatu. Pia, imewakamata watuhumiwa 66 wanaohusika na uhalifu huo. Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema hayo akizungumza za waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kutoa taarifa ya operesheni zilizofanyika mwishoni mwa Desemba 2025.

Lyimo amesema mamlaka hiyo ilifanya operesheni katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Njombe, Kigoma na Arusha. Katika msako huo, wamekamata dawa za kulevya aina ya heroini gramu 37, skanka kilo moja, bangi kilo 7,969 na mirungi kilo 1,363 na kuteketeza ekari 14 za mashamba ya bangi.

Lyimo amesema katika ukaguzi uliofanyika Dar es Salaam kwenye kampuni za usafirishaji wa mizigo, paketi 20 za dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilo 9.5 zilikamatwa, zikiwa zimefungwa kama majani ya mwarobaini yaliyokaushwa. SOMA: Watano washtakiwa usafirishaji wa madawa ya kulevya

Kadhalika, DCEA katika operesheni yake iliyofanyika Temeke, Dar es Salaam katika Mtaa wa Wailes zilikamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilogramu 20 zikiwa zimefichwa ndani ya balo la mitumba na kufichwa kwenye basi la Kampuni ya King Masai Tours lenye namba za usajili wa nchi ya Msumbiji namba AAM 297 CA.

Lyimo amesema basi hilo hufanya safari zake kati ya Nampula nchini Msumbiji na Tanzania na watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni Amasha Mrisho (40), mkazi wa Buza na Seleman Ally (32), raia wa Msumbiji. Operesheni nyingine ilifanyika Sinza C Mtaa wa Bustani Nyumba Namba 16 ambako Jefferson Mwende (35), raia wa Kenya alikamatwa akiwa na gramu 131 za heroini.

Mtuhumiwa huyo aliishi Tanzania tangu 2023 na kutumia biashara ya kuuza chai kuficha biashara ya dawa za kulevya aliyokuwa anaifanya. Aidha, katika eneo la Kinyerezi, Mtaa wa Majoka, Wilaya ya llala watuhumiwa Erick Ndagwa (32), Pau Henry (34) na Tido Mkude (35) walikamatwa na kilo 193 za bangi walizokuwa wanasafirisha kutoka Morogoro kwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *