
Afrika Kusini, imetetea hatua ya kushirikiana na Urusi, Iran na China kwenye mazoezi ya kijeshi Baharini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mazoezi hayo ya wiki moja, kwa mujibu wa Afrika Kusini, yanalenga kuhimiza amani, na inakuja siku chache baada ya Marekani kuzuia na kukamata meli ya mafuta ya Venezuela katika Bahari ya Atlantic.
China inaongoza mazoezi hayo, ambayo yanaonekana kutuma ujumbe kutoka nchi za BRICS kwenda kwa nchi za Magharibi hasa Marekani.
Kaptain Nndwakhulu Thomas Thamaha, amesema hatua hiyo inaonesha uwezo wa nchi hizo kufanya kazi pamoja, wakati huu Marekani ikiyashtumu mataifa ya BRICS kuwa na sera dhidi yake.
Mazoezi haya yaliyopewa jina la Mosi, yalikuwa yameratibiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka uliopita, lakini yakaahrishwa kufuatia mkutano wa G20 uliofanyika jijini Johannesburg, lakini ukasusiswa na Marekani.
Mwaka 2023, mataifa ya Magharibi yaliishtumu Afria Kusini kwa kufanya mazoezi mengine na Urusi na China, wakati wa maadhimisho wa mwaka mmoja, baada ya Moscow kuivamia Ukraine.