“Iran ina matatizo makubwa,” Donald Trump amesema siku ya Ijumaa kuhusu maandamano ya kupinga serikali ambayo yamezuka nchini umo, na kusababisha kukatika kwa intaneti kote nchini na malaka kutumia ukandamizaji kama nji ya kuzima maandamano hayo. “Inaonekana kwangu kwamba watu wameanza kudhibiti baadhi ya miji, jambo ambalo hakuna mtu angefikiria linawezekana wiki chache zilizopita. Tunafuatilia hali hiyo kwa karibu sana,” rais wa Marekani ameongeza.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Ingelukuwa bora msianze kufyatua risasi, kwa sababu tutafyatua risasi pia,” Trump ameonya mamlaka ya Iran. “Ikiwa wataanza kuwaua watu kama walivyofanya hapo awali, basi tutaingilia kati,” rais huyo wa Marekani kutoka chama cha Republican amesema, na kuongeza: “Hiyo haimaanishi kwamba tutatuma wanajeshi nchini Iran, lakini inamaanisha tutawapiga vikali sana, pale inapouma.”

Mamlaka ya Iran imeweka imezima intaneti karibu kabisa kote nchini ili kuzuia usambazaji wa picha na upangaji wa maandamano. Licha ya haya, siku ya 13 mfululizo ya maandamano inaendelea. Ukandamizaji huo tayari umesababisha vifo vya watu wengi tangu kuanza kwa maandamano, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali. Wito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu unaongezeka kimataifa.

Harakati za maandamano, zilizoanza mwishoni mwa mwezi Desemba 2025 kwa sababu za kiuchumi, zimebadilika na kuwa harakati kubwa ya kupinga serikali. Maandamano mapya dhidi ya utawala yalifanyika siku ya Ijumaa jioni nchini Iran, hasa mjini Tehran, ambapo wakazi waliandamana katika barabara kuu kadhaa za jiji.

Angalau watu 62 wameuawa katika maandamano hayo na ukandamizaji wa utawala tangu maandamano hayo yaanze, kulingana na shirika la haki za binadamu la Iran HRANA.

Ayatollah Ali Khamenei amewashumu waandamanaji, akizishushia lawama Marekani na Israel kwa kuingilia kati, na akasema kwamba utawala huo hautarudi nyuma. Amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu “haitarudi nyuma” mbele ya wimbi la maandamano.

Maandamano hayo yalianza na kukabiliana na hali mbaya ya kiuchumi

Mwishoni mwa mwezi Desemba, wafanyabiashara katika Grand Bazaar ya Tehran walifunga biashara zao kupinga uchumi unaozorota, mfumuko wa bei uliokithiri (zaidi ya 50%), na kuanguka kwa rekodi kwa sarafu ya nchi hio rial. Hali ya kiuchumi ilizidishwa na kuwekwa tena kwa vikwazo vya kimataifa. Harakati hiyo ilienea haraka hadi katika vitongoji na miji mingine kama Karaj na Hamedan, ikiwa na kaulimbiu dhidi ya serikali na utawala wa Kiislamu. Muda si muda, maandamano hayo yalizidi utawala huo, ambao kisha uliamua kuanzisha msako mkali na kuzma intaneti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *