
Wairani wameendelea kuingia mitaani katika maandamano makubwa zaidi kote nchini humo ya kupinga ugumu wa maisha katika taifa hilo la Jamhuri ya Kiislam.
Maandamano hayo yanaendelea licha ya mamlaka katika taifa la mashariki ya kati kuzima intaneti kama sehemu ya kuyadhibiti maandamano hayo ambayo mpaka sasa yanatajwa kusababisha vifo vya watu wengi.
Akiyazungumzia maandamano hayo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwake Januari 3, Kiongozi mkuu wa Iran Ali Khamenei amewaita waandamanaji hao kuwa ni waharibifu na wahalifu na kuishutumu Marekani kwa kuichochea hali hiyo.
Siku ya Ijumaa, Rais wa Marekani Donald Trump alitishia tena kwa mara nyingine kwamba nchi yake itafanya mashambulizi ya kijeshi ikiwa waandamanaji wa amani nchini Iran watauawa.