Mamlaka nchini Iran imeendelea kufungia huduma ya Intaneti nchini humo kama sehemu ya kuwadhabibiti waandamaji ambao wako barabarani kupinga kile wanachodai kuwa ni ugumu wa maisha.

Shirika la kimataifa la ufuatiliaji wa intaneti la NetBlocks limesema kwamba “vipimo vyake vinaonyesha kuwa kukatika kwa intaneti kote nchini kunaendelea kutumika hata baada ya saa 36, ​​na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Wairani kuwasiliana na kujua usalama wa wapendwa wao.

Serikali ya Iran imefunga kabisa huduma hiyo kwa watu wote isipokuwa tu kwa vikosi vyake vya usalama na vyombo vya habari vya serikali vilivyochaguliwa.

Kiongozi mkuu wa Iran ⁠Ali ‍Khamenei amewaita waandamanaji hao kuwa ni waharibifu na wahalifu na kuishutumu Marekani kwa kuichochea hali hiyo. Duru zinaeleza kuwa maandamano hayo yaliyoanza wiki mbili iliyopita yamesababisha vifo vya watu wengi nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *