
Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kusisitiza madai yake ya kutaka kukinyakua kisiwa cha Greenland, akisema Marekani lazima ichukue hatua hiyo ili kuzuia China au Urusi kupata udhibiti wa kisiwa hicho muhimu cha Aktiki.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla katika Ikulu ya White House, Trump amesema Washington itafanya “kitu” kuhusu Greenland, iwe wengine wanapenda au la. Kwa sababu isipofanya hivyo, Urusi au China itachukua Greenland, na haitaki Urusi au China kuwa jirani yake.
Kisiwa hicho cha kimkakati ni cha mshirika wa NATO,Denmark na matamshi ya Trump yamezua wasiwasi kote katika nchi za Umoja wa Ulaya na Denmark yenyewe imeweka wazi kwamba Greenland ni kwa ajili ya watu wa kisiwani humo na kwa ajili yao na kwamba wao pekee ndio wanalo jukumu la kuamua hatma ya kisiwa hicho na sio vinginevyo.
Kisiwa cha Greenland kimefunikwa zaidi na barafu na kina idadi ya watu wapatao 57,000.