Gavana wa mji wa Aleppo nchini Syria Azzam al-Gharib amesema hii leo Jumamosi kwamba mapigano yanayoendelea katika vitongoji vya Wakurdi kaskazini mwa Syria yamewafanya takribani watu zaidi ya 155,000 kuyakimbia makazi yao.

Akizungumza na vyombo vya habari gavana huyo ameongeza kwamba idadi kubwa ya watu hao ni wakaazi wa wilaya inayofahamika kama Sheikh Maqsud.

Mapema hii leo yaliripotiwa mashambulizi makali kati ya vikosi vya serikali yaliyofanyika usiku kucha baada ya muda wa mwisho uliowekwa na Syria kwa wapiganaji wa Kikurdi kusitisha mapigano na kujiondoa katika eneo hilo kupita.

Jeshi la Syria limetangaza kwamba kwa sasa limefanikiwa kukamilisha udhibiti wa kiusalama katika eneo la Sheikh Maqsud ingawa Wakurdi wamekanusha madai hayo.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *