Hayo yanajiri huku serikali ya mpito ya Caracas ikichukua hatua ya kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.

Kuachiwa kwa wafungwa hao kulikoanza siku ya Alhamisi wiki hii, kumefanyika kwa mara ya kwanza tangu rais wa mpito Delcy Rodriguez, alipochukua  madaraka baada ya vikosi vya Marekani kuivamia nchi hiyo na kumkamata rais Nicolas Maduro na mkewe, waliosafirishwa Marekani na kufunguliwa mashitaka ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Trump anayemuunga mkono Rodriguez, amesema anaridhika na uongozi wake na muhimu zaidi ni pale Washington itakapopatiwa nafasi ya kufikia hifadhi kubwa ya mafuta ya Venezuela.

Hadi sasa Venezuela imewaachia wafungwa 21 wakiwemo wanasiasa wa upinzani. Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanakadiria kuwa wafungwa 800 hadi 1200 wa kisiasa wapo nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *