Afisa mmoja wa Israel ambaye hakutajwa jina na mwanadiplomasia wa kiarabu, wamesema jeshi la Israel IDF limeweka mipango ya kuanzisha tena operesheni zake za kijeshi Gaza mwezi Machi.

Makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yamekuwepo tangu Oktoba 10 mwaka uliopita, baada ya makundi hayo hasimu, Israel na Hamas kukubaliana na mpango wa vipengele 20 wa Marekani wa kusitisha mapigano katika eneo hilo yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Hata hivyo maafisa hao wanasema operesheni ya Israel haiwezi kufanyika bila kuungwa mkono na Marekani ambayo inajaribu kuzishinikiza pande zote kuingia katika awamu ya pili ya majadiliano ya amani.

Katika makubaliano hayo Hamas inatarajiwa kuweka chini silaha zake huku kikosi cha kimataifa kikipelekwa katika Ukanda wa Gaza kusisimamia ulinzi na usalama wa ardhi hiyo ya Wapalestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *